12 Aprili 2022 - 17:40
Sana'a: UN ihitimishe ukiukaji mkubwa wa usitishaji vita wa muungano Saudia

Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ametaka kuhitimishwa ukiukaji wa usitishaji vita huko Yemen unaofanywa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muhammad Abdulsalam amewasilisha ombi hilo katika mazungumzo yake na Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen. 

Muungano vamizi wa Saudia na Imarati umekiuka mara 1647 usitishaji vita uliofikiwa huko Yemen; ikiwa imepita wiki moja tangu kufikiwa mapatano hayo. Mapatano ya kusitisha vita Yemen yalianza kutekelezwa tarehe Pili mwezi huu sasa moja usiku kwa wakati wa Yemen.   

Muhammad Abdulsalam ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: Katika mazungumzo hayo, tumemtaka Hans Grundberg Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa akomeshe ukiukaji wa mapatano ya kusitisha vita unaofanywa na muungano vamizi wa Saudi Arabia; na pia tumemuomba aanze kuchunguza faili la masuala ya kibinadamu ya Yemen.  

Muhammad Abdulsalam ameongeza kuwa: Katika mazungumzo hayo wamejadili pia udharura wa kuwezesha mchakato wa safari za ndege kutoka uwanja wa ndege wa Sana'a na kurahisisha meli za misaada ya kibinadamu kuingia Yemen bila ya vizuizi au ukwamishaji wowote. 

342/